21 Julai 2026 - 10:44
Hezbollah, Ansarullah na Iran Wampongeza Khalil Al-Hayya kwa Kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas

Hezbollah ya Lebanon, Ansarullah ya Yemen, Kata’ib Hezbollah ya Iraq pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran wametoa pongezi kwa Dkt. Khalil Al-Hayya kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti mpya wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Hamas, wakisisitiza kuendelea kwa Mshikamano na Harakati ya Upinzani wa Palestina licha ya kuuawa kwa viongozi wake wakuu.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Harakati ya Hezbollah ya Lebanon, Harakati ya Ansarullah ya Yemen, Dkt. Kata’ib Hezbollah ya Iraq pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimetoa salamu za pongezi kwa Dkt.Khalil Al-Hayya kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti mpya wa ofisi ya kisiasa ya harakati ya hamas.

Dkt. Khalil Al-Hayya amechaguliwa kushika nafasi hiyo baada ya kuuawa Shahidi Kiongozi wa Hamas, Yahya Sinwar, huku viongozi na taasisi mbalimbali za mhimili wa upinzani zikisisitiza kuwa mauaji ya viongozi hayawezi kukomesha harakati ya Palestina wala kuvunja mshikamano wa wapigania uhuru.

Katika taarifa yake, Hezbollah ilimpongeza Khalil Al-Hayya kwa kumtaja kuwa ni Mujahid na mpiganaji mwenye heshima, pamoja na viongozi na wapiganaji wa Hamas, kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati hiyo.

Hezbollah imesema kuwa uchaguzi huo umetuma ujumbe wa wazi kwa adui wa kizayuni, waungaji mkono wake na wote waliowahi kutegemea kumalizika kwa upinzani wa Palestina, kwamba hamas bado ipo, ina nguvu na ina umoja, na itaendelea na njia yake licha ya mauaji ya viongozi wake na majaribio ya kuvunja azma ya harakati hiyo na wananchi wa Palestina.

“Bendera ya Upinzani, ambayo adui anajaribu kuiangusha kwa kuwaua viongozi wake, itaendelea kuinuliwa juu na kubebwa na watu waaminifu wanaolinda amana na kuendeleza njia kwa imani, azma na uthabiti,” taarifa hiyo ilieleza.

Hezbollah pia imemtakia khalil al-hayya mafanikio na uongozi kutoka kwa mwenyezi mungu katika kutekeleza jukumu hilo kubwa na kubeba amana iliyoachwa na viongozi waliouawa shahidi.

Aidha, Hezbollah imesisitiza kuwa upinzani wa Palestina umejengwa juu ya wananchi wake, ambao, kwa mujibu wa taarifa hiyo, wameandika historia kubwa ya ustahimilivu na kujitolea mbele ya kile ilichokiita mashine ya mauaji na ugaidi ya kizayuni.

Taarifa hiyo imehitimisha kwa kusisitiza kuwa wananchi wa palestina wataendelea kusimama imara katika kulinda haki zao hadi kufikiwa kwa ukombozi wa ardhi yao na maeneo yao matakatifu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha